Rais Samia kuzindua miradi ya Bil. 8.8

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua miradi miwili yenye thamani ya zaidi ya sh 8.8 bilioni katika ziara yake ya siku mbili mkoani tabora kuanzia oktoba 17 hadi 18,2023.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dk Batilda Burian amesema Rais ataingia Mkoani hapo jumanne na kulakiwa na wananchi na viongozi Mjini Igunga.

Dk Burian amesema akiwa katika chuo cha VETA , Rais Samia Suluhu atazindua chuo hicho kilichogharimu sh2.6 bilioni kikiwa kinatarajia kuanza kuchukua wanafunzi januari 2024 na baadaye atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara mjini igunga kabla ya kuelekea nzega.

Ameleeza kuwa akiwa nzega atazindua shamba la mbegu bora linaloendeshwa kisasa lililogharimu sh6.2 bilion ambalo linazalisha mbegu bora za kilimo na baadae kuzungumza na wananchi katika uwanja wa samora mjini Nzega.

Dk Burian amesema awali ilikuwa pia akazindue miradi katika wilaya za urambo na kaliua lakini kutokana na ratiba kubana maeneo hayo hatakwenda na yatapangiwa muda mwingine.

Ziara ya Rais Samia Mkoani Tabora inakuja baada ya kupita miezi 17 tangu alipofanya ziara yake mei 2022 alipotembelea wilaya za uyui, sikonge na Tabora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *