Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Rais Samia Ahutubia Mkutano wa BRICS

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kutokana na kuongezeka kwa changamoto za kiulimwengu, kuna haja ya kuwa na majadiliano mapana yenye lengo la kutafuta suluhisho kwa changamoto ambazo nchi zinapitia, kwa mtu mmoja mmoja na kama taifa.


Rais Samia Ameeleza hayo huko Johannesburg, Afrika Kusini, wakati akihutubia mkutano wa Brics uliowakutanisha viongozi kutoka mataifa zaidi ya 50 duniani zikiwemo nchi wanachama wa Brics Za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini.

Amesema jambo ambalo analiona kama sababu ya majadiliano ni wito wa kuwa na mazungumzo na kuchukua hatua kukabiliana na changamoto hizo ili kukuza uwezo wa kifedha, uwekezaji, biashara na ushirikiano wa kiuchumi.
Rais Samia Amesema Brics inatoa nafasi ya kuja na mikakati ya haki na usawa katika kushughulia masuala ya kiuchumi kupitia ushirikiano wake na bara la afrika. ameongeza kwamba kuna haja ya kuuimarisha Umoja Wa Mataifa (UN) ili kuongeza ushirikiano wa mataifa katika masuala mbalimbali.


Alisema ikiwa imefikisha miaka 78, un kimekuwa ni chombo muhimu kwa wanachama wote. “Tanzania, kwa sababu hiyo, ingependa kupaza sauti kwamba kuna haja ya kubadilisha baraza la usalama la umoja wa mataifa kulifanya liwe na uwakilishi wa haki, thabiti na linaloakisi hali halisi za siasa za kijiografia za sasa”.
Amesema matarajio ya Tanzania ni kuona kwamba masuala ya Afrika na vipaumbele vyake yaendelee kuchukua nafasi kwenye mikutano ijayo ya Brics. Na Tanzania inaunga mkono ushirikiano wa mataifa ulio jumuishi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *