RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI ETHIOPIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili (Februari 15-16, 2025), jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, kushiriki Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).

Mkutano huo, unatarajia kuchagua Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika kwa mwaka 2025 atakaechukua nafasi ya Mwenyekiti wa sasa, Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania.

Aidha, Mkutano huo pia utachagua Viongozi wapya wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ikiwemo Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna sita.

Mkutano pia utajadili Taarifa ya Ushiriki wa Umoja wa Afrika kwenye Mkutano waNchi Tajiri Duniani (G20), Utekelezaji wa Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika na Taarifakuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

Mbali na masuala hayo, Mkutano utajadili ajenda kuhusu Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia iliyopendekezwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kabla ya kushiriki Mkutano wa 38, Rais Dkt. Samia atashiriki Mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika utakaofanyika tarehe 14 Februari, 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *