Rais Samia – Hatufahamu mahitaji ya soko

Rais Samia Suluhu Hassan amekiri kuwepo kwa changamoto ya masoko ya bidhaa zinazozalishwa, lakini Serikali imefanya tafiti na kugundua kuwa kinachopelekea changamoto hizo ni kutofahamu mahitaji halisi ya soko la ndani na nje ya nchi, muunganiko wa soko la bidhaa pamoja na mkulima.

Rais Samia ameyasema hayo leo Alhamisi Septemba 7, 2023 akizungumza katika mdahalo wa vijana na kilimo Ambapo amesema katika suala la muunganiko wa soko na mkulima, Serikali imeanza kuweka jitihada hizo kwa baadhi ya mazao kama korosho ambapo imekuwa na matokeo chanya kwa kusaidia kupandisha bei ya korosho kwa kumjengea mkulima ushirika wa moja kwa moja wa soko la bidhaa hiyo kwa kumuondoa mtu wa kati dalali.

Vilevile Rais Samia amesema jitihada zingine Serikali inazochukua ni kuboresha miundombinu ya usafirishaji kwa kujenga barabara zinazounganisha mikoa-mikoa, mikoa -wilaya zake na barabara kuu na nchi za Jirani ili kuyafikia masoko ya nchi jirani kwa kusaidia mazao kutolewa shambani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *