Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuapisha CPA. Amos Gabriel Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.
Uapisho huo, umefanyika hii leo Agosti 26, 2025 ambapo Rais Samia pia amewataka Wakuu wa Mikoa kuwa karibu na Wananchi, ili kuzifahamu kero zao.

Amesema, “nitoe wito kwa Wakuu wa Mikoa kwamba wanatakiwa kuhakikisha wanakuwa karibu na wananchi ili kuzifahamu kero zao na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na watendaji wengine.”

Katika hafla hiyo ya uapisho, Rais Samia pia amemuapisha Dkt. Deo Osmund Mwapinga kuwa Balozi.


