Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia mitandao yake ya Kijamii amewapongeza Wasanii wa michezo ya sarakasi kutoka Tanzania Ibrahim na Fadhili Ramadhan wanaounda kundi la The Ramadhan Brothers ambao wameibuka Washindi wa mashindano ya kusaka vipaji ya America’s Got Talent Fantasy League usiku wa kuamkia leo yaliyofanyika Nchini Marekani na kujinyakulia kitita cha $250,000 ambazo sawa na Shilingi za Kitanzania milioni 637.5 pamoja na tuzo.
Rais Samia amesema Vijana hao wanaitangaza Tanzania vizuri, ambapo amesema “Pongezi kwa Vijana wetu Fadhili na Ibrahim (The Ramadhani Brothers) kwa kuibuka Washindi katika mashindano ya sanaa na burudani ya AGT: Fantasy League, safari yenu inaendelea kudhihirisha kuwa juhudi, nidhamu, kujituma na kujiamini ni nguzo muhim kufikia mafanikio, mnaitangaza vyema Nchi yetu na kuweka mano bora kwa wengine’ – Rais Samia.