Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Rais Samia awapandisha vyeo maafisa wa polisi 155.

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Samia Suluhu Hassan amewapandisha vyeo maafisa wa polisi 155.

Waliopandishwa vyeo ni pamoja na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi kuwa Manaibu Kamishna wa Polisi 27 na Makamishna Wasaidizi wa Polisi kuwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi 128 ambao wamekula kiapo cha utii kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na kiapo cha maadili ya viongozi wa umma.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Camillus Wambura amesema kupandishwa vyeo kwa maafisa hao kutaongeza chachu ya utendaji kazi, kutenda haki, uadilifu na nidhamu na pia wananchi wategemee mabadiliko makubwa ya kiutendaji.

Miongoni mwa waliopandishwa vyeo ni maafisa nane wa kike ambao wamepanda vyeo na kuwa Manaibu Kamishna wa Polisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *