RAIS  SAMIA AWAPA MKONO WA EID WATOTO YATIMA, WAZEE SHINYANGA

Rais  wa jamuhuri ya muungano wa Tanania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi mbalimbali kwa Makao ya Watoto Yatima (Shinyanga Society For Orphans) iliyopo Bushushu na Makazi ya Wazee na  Wenye Mahitaji Maalum Kolandoto iliyopo Kata ya Kolandoto hatika  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitr.

Akizungumza baada ya kukabidhi kwa niaba yake  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Anamringi Macha amesema Rais Samia anatambua, anathamini na kuheshimu uwepo  wao na kwamba yeye mwenyewe na Serikali yake anawapenda na kuwajali wakati wote ndiyo sababu ya kuwapelekea zawadi hizo kwani wao pia ni jamii kama ilivyo jamii nyingine na wanazo haki sawasawa kama binadamu wengine.

“Tunahitimisha Mfungo Mtukufu wa Mwezi wa Ramadhan na kushrehekea sikuku ya idd elftir  nimeelekezwa na rais Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niwaletee zawadi zake alizotoa maalum kwa ajili yenu ili katika kusherehekea Sikukuu hii ya Eid Al – Fitr muweze kufurahi pamoja naye kupitia zawadi hizi,” alisema RC Macha.

“Mheshimiwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan anatambua, anathamini na kuheshimu uwepo wenu na kwamba Serikali anayoiongoza itaendelea kuwa karibu na kuishi nanyi wakati wote, aidha itaendelea kusaidizana nanyi katika nyanja na nyakati mbalimbali kutegemea na mahitaji ya wakati husika pia,” alisisitiza RC Macha.

Kwa nyakati tofauti Mkurugenzi wa Makao ya Watoto Bibi Haiyamu Said na Msimamizi wa Makazi ya Wazee na Wenye  Mahitaji Maalum, Sophia Kang’ombe wamemshukuru sana. Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwathamini, kuwajali na hata kuwapatia zawadi mbalimbali nyakati zote kupitia wasaidizi wake (Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga) na kwamba wao wanamuombea kwa Mwenyezi Mungu awe na afya njema wakati wote ili andelee kuwahudumia wao na Watanzania wote.

Huu ni muendelezo na utaratibu wa  Rais Dr Samia Suluhu Hassan wa kutoa zawadi na mahitaji mbalimbali kwa makundi mbalimbali ambapo kwa leo Makao ya Watoto Yatima (Shinyanga Society For Orphans) chenye jumla ya watoto 23 huku Makazi ya Wazee na Wenye Mahitaji Maalum Kolandoto kina wazee 18 wamepokea mahitaji mbalimba;I katika kusherekea sikukuu ya idd elfitir.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *