Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Rais Samia atoa wito kwa wazazi

Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan amesema kupitia tamasha la Kizimkazi la mwaka 2023 serikali imezindua miradi mbalimbali ikiwemo elimu ambapo madarasa 11 yamefunguliwa katika shule ya msingi kizimkazi na kufanyiwa marekebisho na tasaf tangu ilipojengwa mwaka 2010.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi katika siku ya kilele cha tamasha hilo Unguja, Zanzibar na kuongeza kuwa katika kijiji cha muyuni madarasa 6 pia yamefanyiwa ukarabati na kujengwa chumba kikubwa cha mitihani katika shule ya sekondari Muyuni.

Aidha Dokta Samia amesema katika sekta ya afya wamezindua kituo cha afya kipya kilichojengwa na wafadhili kutoka Oman cha afya ya mama na mtoto kitakachorahisisha upatikanaji wa huduma kwa mama wajawazito na watoto pamoja na kuzindua miradi mingine ya maji, utalii na viwanja vya michezo kwa watoto.

Rais Dokta Samia pia amesisitiza kurithishwa mila na desturi zenye maadili mema kwa watoto ikiwemo lugha ya taifa ya kiswahili, tamaduni ya vyakula na tamaduni za ngoma kufuatia kauli mbiu ya mwaka huu ya tamasha la kizimkazi isemayo tuwalinde kimaadili watoto wetu kwa maslahi ya taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *