Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Rais Samia atoa wito kwa viongozi wa Dini

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali inatambua na kuthamini mchangao unaotolewa na taasisi pamoja na mashirika ya kidini nchini kutokana na kazi kubwa ya maendeleo katika nyanja mabalimbali iwemo elimu, afya, maji na kilimo.

Akizungumza katika ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la kanisa la Anglikana Centre (Safina House) mkoani Dodoma rais Samia amepongeza kanisa hilo kwa jitihada za kubeba jukumu la kilimo na kuwa msaada kwa serikali katika utekelezaji wa programu ya jenga kesho iliyo bora kwa vijana kujihusisha na shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi.

Aidha Dokta Samia amehimiza viongozi wa dini kulinda maadili na kukemea maovu katika jamii ili kuwa na taifa lenye watu waadilifu na kuendelea kuliweka taifa katika mikono salama ya mwenyezi mungu kudumu katika umoja, amani na mshikamano.

Lengo la ujenzi wa jengo hilo lenye mfanano wa meli ya safina ya nuhu lililofunguliwa rasmi leo ni kupangisha na kupata fedha ili kuendesha shughuli mbalimbali za kikanisa za kuhubiri injili na kutoa huduma kwa jamii ikiwemo elimu, afya na maendeleo ya jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *