Rais Samia atoa Mil. 10 kwa Twiga Stars

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi ya shilingi milioni 10 kwa wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, baada ya kuwatoa Ivory Coast kwa mikwaju ya penati katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON kwa wanawake na kusonga mbele.

Aliyetoa taarifa hiyo ni katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson msigwa aliyekuwepo Azam Complex, Chamazi akishuhudia mechi hiyo ya marudiano iliyomalizika kwa matokeo ya jumla ya 2-2.

FT: Tanzania 2-0 Ivory Coast (Agg: 2-2, Pen: 4-2).

Kituo kinachofuata ni mshindi kati ya Togo au Djibouti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *