RAIS SAMIA ATOA MAJIBU MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Mchakato wa Katiba Mpya utatekelezwa katika kipindi kijacho cha miaka mitano.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Juni 27, 2025 wakati akihutubia Bunge jijiji Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kulivunja kwa aajili ya maandalizi ya uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 2025.

Amesema, “mchakato wa Katiba mpya ni miongoni mwa ahadi ambazo zinaonekana katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2025/2030.”

Rais Samia ameongeza kuwa, “shughuli ya kuanza kufanya Katiba mpya itatekelezwa katika kipindi kijacho cha miaka mitano.” – Rais Samia Suluhu akitoa hotuba ya kuvunja Bunge la 12”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *