Rais Samia atoa heshima za mwisho kwa Zelothe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amefika kutoa heshima za mwisho nyumbani kwa aliyekuwa Kamishna Msaidizi mwandamizi (mstaafu) wa Jeshi la polisi nchni, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha, Marehemu Zelothe Stephen Zelothe Seaview-Upanga jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28,2023.

Zelothe aliyewahi kukitumikia chama na serikali katika nafasi mbalimbali akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, alifariki Octoba 26, 2023 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mara ya kwanza marehemu Zelothe, alichakuguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Desemba 2019, akichukua nafasi ya Loota Sanare ambaye aliteuliwa na Rais wa wakati huko, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, akichukua nafasi ya Dk Stephen Kebwe ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Hata hivyo, Novemba 2022 Kamanda Zelothe alifanikiwa kuitetea nafasi yake na hivyo kuendelea kuongoza chama hicho mkoani Arusha mpaka mauti ilipomkuta.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *