Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya hekta 5,000 kwa wakazi wa Idosero wilayani Bukombe mkoani Geita ili kumaliza mgogoro baina ya wananchi hao na hifadhi ya shamba la miti Silayo uliodumu kwa zaidi ya miaka thelathini huku serikali ikiwataka wananchi waliojenga nyumba katika hifadhi hiyo wahamie katika eneo waliopewa.

Wakizungumza na Jambo Fm baadhi ya wakazi hao wameeleza furaha yao kwa kupatiwa eneo hilo na kuipongeza serikali kwa kutatua mgogoro ambao umedumu kwa mda mreu hali ambao ilikuwa imejenga chuki kubwa kati yao na wahifadhi wa shamba la miti Silayo.
Mhifadhi mkuu wa shamba la miti Silayo Juma Mwita amewataka wananchi waliopatiwa eneo hilo kuendela kutunza mazingira pamoja na kutovamia maeneo mengine ya hifadhi ili kulinda hifadhi hiyo nakutunza mazingira na shamba hilo ili liwe endelevu.


