Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, uhamisho na mabadiliko ya viongozi mbalimbali akiwemo Afisa Tarafa ya Ilemela, Godfrey Eliakimu Mnzava kuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi.
Mnzava anachukua nafasi iliyoachwa wazi na James Wilbert Kijaji aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka uteuzi, uhamisho namabadiliko hayo ni kama inavyoonekana katika viambata.