RAIS SAMIA AMUWAJIBISHE CHALAMILA KWA KUTOA KAULI YA KUMFEDHEHESHA MWANAMKE – LHRC

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimearifu kusikitishwa na kauli za kufedhehesha na kutweza utu wa Mwanamke, nyingine zakutatanisha zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa umma kinyume namaadili na miiko ya utumishi wa umma.

Taarifa iliyotolewa na kituo hicho kupitia kwa Mkurugenzi wake Dkt. Anna Henga imeeleza kuwa,kauli hizo pia zipo kinyume na haki za binadamu na misingi yautawala bora.

“Ndugu waandishi wa habari,Mwishoni wa juma lililopita ilisambaa picha mjongeo kupitia vyombo vyahabari ikimnukuu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ndugu Albert Chalamila, wakati akihutubia wananchi katika moja ya hafla wilayani Temeke jijini Dar es Salaam,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, imeeleza kuwa, katika video hiyo, Chalamila alionekana akisema kuwa alipokea malalamiko kutoka kwa mama mmoja aliyelalamikia huduma zisizoridhisha kutoka moja ya hospitali zilizopo mkoa wa Dar es Salaam alipokwenda kujifungua.

“Mama huyo alidai kutozwa fedha kwa ajili ya huduma yakujifungua na ndipo akaamua kuwasilisha malalamiko yake kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na wakati akimjibu mama huyo ndugu Chalamila alinukuliwa akisema (toka nje chukua bajaji nenda zako nyumbani kamwambie mmeo achukue visu na mikasi akusaidie kujifungua),” ilibainishwa.

LHRC imeeleza kusikitishwa na kufadhaishwa na kauli hiyo inayotweza na kufedhehesha utu wa Mwanamke na misingi ya utawala bora kwani Afya ya uzazi ni haki ya kikatiba kama ilivyoanishwa katika ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na mikataba ya Kikanda na Kimataifa ambayoTanzania ni nchi mwanachama.

“Ndugu Waandishi wa habari kwa mujibu wa sera ya afya ya 2007 huduma za msingi za afya, ikiwa nipamoja na huduma za mama na mtoto, zinapaswa kutolewa bure kwa mamawajawazito katika vituo vya afya vya serikali. Hii ni sehemu ya jitihada za Serikali za kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga,” ilifafanua taarifa hiyo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za Wizara ya Afya, changamoto zimekuwa zikijitokeza katika utekelezaji, ikiwemo upungufu wa vifaa vya msingi kamavile mikasi, pamba, glovu, na vinginevyo ambapo kwa mujibu wa sera hiyo ya 2007, huduma za msingi za afya kwa wajawazito na Watoto chini ya umri wa miaka mitano zinapashwa kutolewabila malipo, isipokuwa kwa vifaa vya binafsi kama vikasha vya uzazi (“maternity packs”) vinaweza kuwa jukumu la mama mzazi au familia yake,hasa pale ambapo hospitali haina vifaa vya kutosha.

LHRC imefafanua kuwa, “kwa ujumla Hospitali za umma zinatakiwa kuhakikisha kuwa vifaa vya uzazi vinapatikana kwa ajili yahuduma hii muhimu, ikiwa mama mzazi anaombwa kulipia huduma ambazo zinapaswa kuwa burekatika hospitali za umma, anashauriwa kutoa taarifa kupitia ngazi za uongoziwa kituo cha afya husika au kufikisha malalamiko Wizara ya Afya kupitia simu za mawasiliano zilizotengwa kwa ajili ya malalamiko.

Kwa mujibu wa ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya1977, LHRC imearifu kuwa, viongozi wa umma wanawajibika kwa umma ambao ndiyo wenye dhamana ya Serikali na si kutoa kauli za kuwakebehi kwani si mara ya kwanza kwa Chalamila kutoa kauli zenye mtazamo wakutweza utu, kudhalilisha au kukebehi wananchi hadharani.

“Tunakemea vikali kauli hii na kuwaasa viongozi wa umma kuwa na hadhari pindi wanapotoa matamshi yao kwa wananchi. Hivyo, LHRC inatoa wito ufuatao, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan achukue hatua za kinidhamu dhidi ya ndugu Chalamila. 2. Viongozi wote wa umma kuzingatia utu na kutoa matamshi yenye staha na yenye kuonyesha uwajibikaji wao kwa wananchi kama ilivyoanishwa katika ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania 1977,

“3. Sekretariati ya maadili ya viongozi wa umma imuite na kumhoji nduguChalamila kama hatua za kinidhamu hazitachukuliwa dhidi yake.4. Kuboreshwa kwa mitaala ya ufundishaji katika vyuo vya kada ya afyahasa katika eneo la utoaji wa huduma na matumizi ya lugha zenyestaha na kujali,” alibainisha Dkt. Anna Henga kupitia taarifa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *