Rais Samia amewasili nchini Zambia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Zambia Oktoba 23 kuanza ziara ya kitaifa ya siku tatu nchini humo.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Rais Samia alilakiwa na mwenyeji wake, Rais Hakainde Hichilema na viongozi wengine wa taifa hilo.

Kesho, Rais Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia na keshokutwa anatarajiwa kuwa Rais wa kwanza wa Afrika katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi iliyopita kuhutubia Bunge la Zambia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *