Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt Godwin Mollel leo Februari, 25, 2024 amefika kuwajulia hali majeruhi 21 wa ajali iliyohusisha magari manne eneo la Ngaramtoni, Mkoani Arusha waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mount Meru.


Dkt. Mollel amesema majeruhi wote wanaendelea vizuri na mmoja ndo kapewa Rufaa ya kwenda hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Mara baada ya kuwajulia hali, Naibu Waziri Mollel amesema ‘Rais Samia Suluhu Hassan ametuelekeza majeruhi wote wa ajali hii kupatiwa matibabu bila kulipa gharama zozote” – Dkt. Mollel