Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amelivunja rasmi Bunge la 12 la Tanzania hii leo Agosti 3, 2025.
Uamuzi huo, sasa unatoa fursa kwa uteuzi wa wagombea wa Uchaguzi Mkuu pamoja na kuendelea kwa taratibu za Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29, 2025.
Kuvunjwa kwa Bunge kunatikana na masharti ya Ibara ya 90(2)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambapo baada ya hatua hiyo Bunge halitaruhusiwa kuketi tena hadi baada ya Uchaguzi Mkuu na baada ya kuapishwa kwa wabunge wapya, isipokuwa kwa masharti ya Ibara ya 90(4) ya Katiba.

Aidha, Ibara ya 90(4) inampa Rais mamlaka ya kutoa Taarifa Maalum ya kuitisha Mkutano wa Bunge na kuagiza kwamba Spika pamoja na wote waliokuwa wabunge mara tu kabla ya kuvunjwa kwa Bunge, wahudhurie Mkutano huo iwapo kutatokea hali ya hatari (vita, majanga au maafa makubwa) inayohitaji Bunge kukutana.


