Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya
uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa walioteuliwa ni pamoja na
Arch Dkt. Fatma Kassim Mohamed kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kwa kipindi cha pili.
Wengine ni Balozi Dkt. Jilly Elibariki Maleko aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), akichukua nafasi ya Balozi Begum Karim Taj ambaye amemaliza muda wake.

Prof. Eliakimu Mnkondo Zahabu ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (National Carbon Monitoring Center – NCMC) na Lucas Abrahamani Mwino aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).
Mwino anachukua nafasi ya Dkt. John Kedi Mduma ambaye amemaliza muda wake.


