RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI NA UHAMISHO WA WAKUU WA MIKOA, MAKATIBU TAWALA WAGUSWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya
uteuzi na uhamisho wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa, CP. Salum Rashid Hamduni aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Alexander Pastory Mnyeti ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, huku Stanslaus Haroon Nyongo akiteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Jumanne Abdallah Sagini akiteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Taarifa zaidi kuhusiana na majina ya uteuzi na uhamisho ni kama inavyoonekana katika viambata No. 1&2.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *