Rais Samia afanya uteuzi AICC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Christine Gideon Mwakatobe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) akichukua nafasi ya Ephraim Mafuru ambaye siku tatu zilizopita aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Kabla ya uteuzi huo Mwakatobe alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *