Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesafiri kwa treni ya SGR kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ambapo pamoja na majukumu mengine pia atashiriki zoezi la uboreshaji wa taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura hii leo Mei 17, 2025 katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji, Chamwino Dodoma.



