Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Jaji John Mgeta kusimamia maadili ya Watumishi wa umma kwa kuzingatia miiko inayowaongoza katika kutekeleza majukumu yao.
Agizo la Rais Samia amelitoa wakati wa uapisho wa Viongozi wateule hii leo Mei 24, 2025 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema, “sisi viongozi ni wanadamu, ni watu na ni wanadamu. Tuna miiko tumewekewa, ukitufanyia assessment leo unaweza ukatukuta ni asilimia 30 tunafuata kweli hiyo miiko ya uongozi.”
“Sasa mna kazi ya kutulea huko na kuangalia. Ujazaji tu fomu na kukuleteeni ile tunafanya sana, lakini matendo mengine yetu binafsi huko ni mambo mengine. Kwa hiyo naomba mkasimamie maadili kwenye utumishi wa umma,” aliongeza Rais Samia.