Rais wa Kenya William Ruto, ametuma wataalamu katika nyumba ya marehemu aliyeshikilia rekodi ya dunia ya kukimbia Kelvin Kiptum na kuwapa maagizo ya kumjengea nyumba ya vyumba vitatu mjane na watoto wake.
Ruto amewaagiza wataalamu hao kujenga nyumba hiyo ndani ya siku saba kabla ya mazishi ya mwanariadha huyo kufanyika Februari 24.
Rais Ruto anatarajiwa kusimamia shughuli ya kukabidhi nyumba kwa mjane na watoto wa Kiptum kabla ya marehemu kuzikwa.