Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Kiongozi akitaka kujiuzulu anapaswa kumpa taarifa Boss wake kwanza badala ya kukurupuka kwenda kutangaza kwenye Vyombo vya Habari.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo February 1, 2024 wakati akiwaapisha Mawaziri wapya wateule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ikulu Zanzibar huku akitoboa siri kuwa hata yeye akiwa Waziri wa Ulinzi aliwahi kumwandikia barua ya kujiuzulu Rais Mstaafu Kikwete baada ya mabomu ya Gongolamboto lakini alimwambia ile ni ajali na hana sababu ya kijiuzulu.