Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ametoa msamaha kwa wanafunzi waliopo chuo cha mafunzo wanaotumikia vifunguo vyao gerezani kwa makosa tofauti ambapo taarifa kwa umma iliyotolewa Ikulu ya Zanzibar leo Januari 11, imeeleza jumla ya wanafunzi 33 wamepata msamaha wa rais kwa kuachiliwa huru.
Msamaha wa Rais wa Zanzibar uko chini ya Kifungu cha 59 cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 wa kutoa msamaha kwa mtu aliyehukumiwa kwa kosa lolote na kwa kutumia uwezo wake huo aliopewa Kikatiba, Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kusherehekea Miaka Sitini na Moja (61) ya Mapinduzi ya Zanzibar, amewapatia msamaha kwa kuwaachia huru jumla ya Wanafunzi thelathini na watatu (33) wanaotumikia adhabu zao Chuo cha Mafunzo ambapo kati ya hao Wanafunzi Ishirini na watano (25) kwa Unguja na wanafunzi wanane (8) kwa upande wa Pemba.
Hii ni kawaida ya Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kutoa msamaha kwa baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo katika maadhimisho kama haya.