Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi akifurahia bao la nne la mkwaju wa penalti lililoipa ubingwa Zanzibar Karume Boys kwenye mashindano ya CECAFA kwa vijana chini ya umri wa miaka 15.

Dk Mwinyi alikuwa akifuatilia fainali hiyo ofisini kwake Ikulu Mnazi Mmoja visiwani Zanzibar ambapo Uganda ndio walikuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo.