Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amemteua Mudrik Ramadhan Soraga kuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale.
Kabla ya uteuzi huo uliofanyika leo Jumamosi Januari 27, 2024, Mudrik alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.
Simai alitangaza kujiuzulu kupitia video iliyosambaa mitandaoni usiku wa kuamkia Januari 26, 2024, akidai amejiuzulu kutokana na mazingira yasiyo rafiki ya kazi.