Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Mheshimiwa Shariff Ali Shariff kuwa Waziri wa Nchi; Ofisi ya Rais, Kazi,Uchumi na Uwekezaji.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena A Saidi inasema Mheshimiwa Shariff ataapishwa tarehe 22 Februari, 2024 Saa 8:00 mchana katika Ukumbi wa Baraza la Mapinduzi – Ikulu, Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza leo tarehe 21 Februari, 2024.