
Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin ametaka kukutana nae haraka iwezekanavyo na mazungumzo hayo yatahusu vita ya Urusi na Ukraine
Trump alinukuliwa akisema “Rais Putin alisema anataka kukutana nami haraka iwezekanavyo,” Trump alisema wakati wa hotuba yake kwenye kongamano la Turning Point’s America Fest. “Kwa hivyo inabidi tungojee hii, lakini tunapaswa kumaliza vita hivyo. Vita hivyo ni vya kutisha, vya kutisha.” – Trump
Trump, ambaye anatarajiwa kurejea Ikulu ya White House mnamo mwezi Januari 2024, hapo awali alisema kwenye kampeni kwamba ikiwa atachaguliwa, anaweza kumaliza vita “Ndani ya Saa 24.”

Trump hivi karibuni alikosoa mabadiliko ya sera ya Rais Joe Biden ambayo yaliruhusu Ukraine kutumia silaha zinazotolewa na Marekani kushambulia ndani ya ardhi ya Urusi.Mapema mwezi huu, Trump alikutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy mjini Paris pamoja na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kabla ya kufunguliwa tena kwa Kanisa Kuu


