Rais wa zamani wa Uruguay,, José “Pepe” Mujica, ambaye pia aliwahi kuwa mpiganaji wa msituni na baadaye kutawala Uruguay (2010 – 2015), amefariki akiwa na umri wa miaka 89.
Taarifa za kifo cha Mujica zimetangazwa na Rais wa sasa wa Uruguay, Yamandu Orsi kupitia andiko lake la mtandao wa X akisema “rais maskini zaidi duniani,” alifariki Mei 13, 2025 kwa maradhi ya Saratani.

“Ni kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha mwenzetu Pepe Mujica. Rais, mwanaharakati, mwamuzi na mwongozaji. “Tutakukumbuka sana, mzee mpendwa,” aliandika Rais Osri.
Mujica, maatifu kama Pepe alipata umaarufu ulimwenguni kote kwa kukataa mikutano akiwa mkuu wa Uruguay, na alikuwa akiendesha gari lake mwenyewe akikataa kuishi katika ikulu ya rais kwa kukaa katika nyumba yake ya kawaida karibu na Montevideo.

