Rais wa Rwanda Paul Kagame amemteua binti yake Ange Kagame(29) kuwa naibu mkurugenzi mtendaji katika ofisi yake,ambaye anayesimamia baraza la mikakati na sera, kwa mujibu wa taarifa za kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoongozwa na Rais Kagame siku ya Jumanne.
Taarifa hiyo pia ilitangaza Uteuzi wa watu wengine wakiwemo Mabalozi wapya wa Ethiopia, Morocco, Misri na Guinea.