RAIS DKT. SAMIA AZUNGUMZA NA RAIS WA GHANA MAHAMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Ghana, John Dramani Mahama, katika Ikulu Ndogo ya Arusha hii leo Machi 2, 2025.

Rais wa Ghana Mahama, amewasili Mkoani Arusha kwa ajili ya Ziara ya Kikazi, ambapo anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mwaka mpya wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.

Pia atahudhuria Sherehe za kumbukizi ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mahakama hiyo mwaka 2006.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *