Rais atoa bilioni 2.7 ushindi wa Equatorial Guinea

Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mbatsogo ametangaza leo Januari 23 ni sikukuu ya kitaifa ili kusheherekea ushindi wa timu yao ya Taifa baada ya kuwafunga waandaji wa AFCON 2023 Ivory Coast magoli 4-0 na kufuzu hatua ya mtoano ya michuano hiyo.

Pia Rais Teodoro katika kusheherekea ushindi huo, ameipa timu hiyo ya Taifa zawadi ya Euro Milioni 1 sawa na shilingi Bilioni 2.7 za kitanzania.

Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea ambaye ni mtoto wa Rais wa nchi hiyo, Teodoro Nguema Obiang Mangue aliahidi kutoa kwa timu kiasi cha Euro 50,000 (Tsh Milioni 136) kwa kila goli litakalofungwa kwenye mchezo wa jana, hivyo ametoa Euro 200,000 (Tsh Milioni 547) kwa magoli manne yaliyofungwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *