Rai wa China aomba Kongamano la Amani Kumaliza Vita Gaza

Rais wa China Xi Jinping Alhamisi ya leo  ameomba uwepo wa kongamano la amani la kumaliza vita kati ya Israel na Hamas, wakati alipokuwa akihutubia viongozi wa kiarabu kwenye kikao kinacholenga kuimarisha uhusiano na mataifa yao.

Xi wiki hiI amekuwa mwenyeji wa rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, na viongozi kadhaa wengine wa kiarabu. Ingawa China ina mafuta yake, kwa muda mrefu imeagiza mafuta ghafi kutoka Mashariki ya Kati, ambako imekuwa ikitaka kupanua ushawishi wake katika miaka ya karibuni.

Pia China imejiweka katika hali ya kutoegemea upande wowote kwenye mzozo kati ya Israel na Palestina, kinyume na hasimu wake Marekani, wakati ikitetea kuwepo kwa suluhisho la mataifa mawili, huku pia ikidumisha uhusiano mwema na Israel.

China pia imeilenga Mashariki ya Kati kama eneo muhimu kwenye mradi wake maarufu wa Belt and Road, katika kuimarisha miundombinu, kama mbinu ya kueneza ushawishi wake kimataifa,kizungumza muda mfupi baada ya hotuba ya XI, Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuhakikisha kuwa wapalestina waliopo kwenye Ukanda wa Gaza hawaondolewi kwenye eneo lao lililokumbwa na mapigano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *