Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha (EFCC)nchini Nigeria, imemfiikisha Mahakamani Pascal Okechukwu, maarufu kama Chief Priest, ambaye ni rafiki wa staa wa muziki Davido, kwa madai ya kuchezea pesa za Nigeria (Naira) katika sherehe aliyohudhuria hivi karibuni.
Chief Priest, anakabiliwa na mashtaka matatu ya kunyunyiza na kuchezea Naira kwenye hafla ya kijamii, kinyume na masharti ya Sheria ya Benki Kuu ya Nigeria ya 2007 na anatarajiwa kupandishwa kizimbani leo mbele ya jaji wa Mahakama Kuu ya Shirikisho katika Jimbo la Lagos.
Hivi karibuni mastaa mbalimbali nchini humo wamejikuta matatani na kukamatwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kosa kuu la kuchezea pesa ya Nigeria.