Wananchi Wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa wametakiwa kuchukua tahadhari za kiusalama ikiwa ni pamoja na kusimamisha Shughuli za Kilimo Kufuatia Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha Maafa.
Hayo yamejiri Mara baada ya Mvua kubwa iliyoambatana na Radi Kusababisha Maafa katika vijiji viwili tofauti wilayani humo ambapo Kijana mmoja aitwaye Edward Ibrahim Silungu mwenye Umri wa Miaka 32 katika Kijiji Cha Muze na Ng’ombe wawili aliokuwa akilimia Shambani kwake kupoteza maisha kwa kupigwa na radi, huku Katika kijiji cha Tamasenga Manispaa ya Sumbawanga Ng’ombe 25 wakifariki kwa kupigwa na radi.
Akitoa Salamu za pole Kwa niaba ya Serikali Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ally Chirukile ametoa wito Kwa wananchi kuchukua tafadhari katika kipindi hiki Cha Mvua kubwa ikiwa ni pamoja na Kuacha kufanya shughuli za Kilimo Kwa Kutumia Ng’ombe Wakati Mvua ikiendelea kunyesha.