![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2024/12/JANABI-1.jpeg)
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Mshauri wa Rais kwenye masuala ya Afya, Profesa Mohamed Janabi kujiandaa kugombea nafasi ya Ukurugenzi wa Shirika la Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Nafasi ambayo alishinda marehemu Dkt.Faustine Ndugulile.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2024/12/NDUGULILE-1024x448.webp)
Dkt. Faustine Ndugulile ambaye pia alikuwa Mbunge wa Kigamboni, alifariki dunia Novemba 27, 2024 akiwa anapatiwa matibabu Nchini India, ikiwa ni miezi michache baada ya kushinda nafasi hiyo.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2024/12/sshh-1024x729.jpeg)
Rais Samia baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali leo Jumanne, Desemba 10, 2024 kwenye Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar, amesema wamepitia wasifu zaidi ya tano kubaini kwamba Profesa Janabi ana sifa ya kurithi mikoba hiyo ya Ndugulile.
Kwenye taarifa yake Rais Samia amesema “Naomba nifichue siri hapa, tumepitia zaidi ya CV tano na tukaona Profesa Janabi anafaa kuchukua nafasi ya Dk Ndugulile. Hivyo, tunakundaa kwenda kugombea nafasi hiyo muda utakapofikia. Ujiandae’’. – Rais Samia.