Prof. Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa ametetea tena nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama cha CUF Taifa baada ya kushinda tena kwenye Uchaguzi Mkuu wa Chama hicho akipa kura 216 kati ya kura halali 592 zilizopigwa huku anayemfuatia Hamad Masoud akipata kura 181.
Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi CUF Taifa amesema “Kwa matokeo haya niliyonayo na kwa nafasi yangu ya Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi namtangaza Ibrahim Lipumba kuwa ndiye Mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa uchaguzi wa CUF, Ndugu zangu kwa Mgombea ambaye hajaridhika na matokeo tunayo Kamati ya Rufani anakaribishwa kuwasilisha rufaa yake kwa Kamati hiyo”
Uchaguzi huo ulikuwa na jumlaya Wagombea 9 akiwemo Ali Juma Khamis ambaye alijitoa baadae, Mgombea wa pili ni Athman Kanali aliyepata kura 5, Hamadi Hamadi kura 181, Juma Shaban kura 6, Maftaha Abdallah Nachuma kura 102, Wilfred Lwakatare kura 78, Ngaitile Siwale kura mbili na Chifu Lutalosa Yemba kura mbili .