PPRA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA ZPPDA KUBORESHA SEKTA YA UNUNUZI NCHINI

MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma nchini (PPRA), imesema itaendelea kushirikiana na serikali ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Ununuzi na Uondoaji Mali za Umma(ZPPDA), katika kuhakikisha jahazi la Ununuzi wa Umma wanauvusha salama lengo likiwa ni kufikia malengo ambayo serikali na wananchi wake wamekuwa wakiyahitaji kila siku.

Hayo yamesemwa leo Januari 27, 2025 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Denis Simba, wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa ajili ya kujifunza kuhusu namna ya PPRA inavyotekekeza majukumu yake.

Amesema kuwa, wamefanikisha maboresho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ikiwa ni pamoja na kupata sheria mpya ya mwaka 2023 na kanuni zeke za mwaka 2024 huku akisema maboresho hayo yameimarisha uwazi na uwajibikaji katika michakato ya Ununuzi.

Mkurugenzi huyo wa PPRA amesema, Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST), ulizinduliwa rasmi mwaka 2024 na kwamba ulianza kutumika mwaka 2023 ambapo umeleta mageuzi makubwa katika Sekta ya Ununuzi wa Umma.

Ameongeza kuwa, mfumo huo unaruhusu michakato ya Ununuzi kufanyika kwa uwazi na ufanisi mkubwa, kuongeza uwezo wa kufuatilia na kudhibiti matumizi ya fedha za Umma.

“Mfumo wa NeST umepata tuzo ya kuwa mfumo bora wa Ununuzi wa Umma kwa ubunifu barani Afrika ,tuzo hii ilitolewa mjini Kampala Uganda na Association for Public Administration and management (AAPAM), chini ya Umoja wa Afrika, ” alisema Simba.

Amesema wamewezesha mfumo wa NeST kukubalika na mashirika makubwa ya kimataifa yakiwamo Benki ya Dunia na Shirika la Maendeleo ya Kilimo (IFAD).

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Manaasha Khamis Juma amesema kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Hussein Ally Mwinyi amejikitaka kwenye miradi mingi na miradi hiyo lazima Sheria ya manunuzi ifanyike.

“Leo tupo katika wizara ya fedha kumekuja kutembelea, tupo na PPRA na sisi tupo na mamlaka kama hii lengo letub tumekuja kuona wenzetu wanafanya nini na hasa na wameendelea kwa kiasi gani, kama Kuna changamoto Lakini pia mafanikio, amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *