Kupitia instastory ya Mwanamitandao Poshy Queen ameamua kuvunja ukimya na kuweka wazi kuwa hajawahi kuwa na mahusianio ya kimapenzi na aliyekuwa Dj wa Harmonize, Dj Seven na wawili hao walikuwa marafiki tu.
“Sikutaka kuzungumzia hili, lakini kwa sasa, kwa ajili yangu na taswira ya mwenzi wangu, kwa dhati kabisa, kamwe sijawahi kutoka kimapenzi na Seven”, ameandika Poshy.
Akaongeza “Alikuwa rafiki na tumefanya kazi pamoja, yeye anajua ukweli. Sina upumbavu huo”.