POLISI YAWATAKA WANANCHI KUWEKA UZIO KWENYE VISIMA NA MABWAWA.

Na William Bundala

KAHAMA

Jeshi la Polisi wilaya ya Kipolisi Ushetu wilayani Kahama Mkoani Shinyaga limewataka wananchi kuweka uzio katika mabwawa na visima walivyochimba ili kuzuia  wimbi la watoto kutumbukia visimani na kwenye madimbwi.

Wito huo umetolewa na Kaimu mkuu wa kituo, Otyeno Onyanya katika kikao cha wakulima wa chama cha misingi Uyogo kilichofanyika katika kata Kijiji cha Uyogo kata ya Uyogo halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

“Tupo katika msimu wa mvua niombe mnifikishie salamu zangu kwa watu wanaochimba madimbwi na visima, waweke uzio kwani tumekuwa tukipata simu nyingi za watoto kudumbukia kisimani,Imarisheni visima vyenu ili kuokoa maisha ya watoto wetu” Amesema Onyanya.

Sambamba hayo Onyanya  amesisitiza kuondolewa kwa mabua ya zao la Tumbaku kwenye mashamba na kuyachoma moto kwani yana madhara makubwa kwa afya ya binadamu.

“Jambo lingine ni Mabua niombe tufuate maagizo ya wataalamu ondoeni mabua ya tumbaku shambani na mchome moto haya mabua yana madhara kwa afya za binadamu” Ameongeza Onyanya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Uyogo Jofrey Kazoya amewataka wakulima wa zao la Tumbaku kuwa waaminifu kwa kupeleka zao lote  la Tumbaku walilozalisha katika Masoko.

“Ndugu wakulima wenzangu najua tupo kwenye msimu wa masoko naomba tuwe waaminifu na tupeleke tumbaku yetu Sokoni ili kuzidi kuainika kwa serikali na taasisi za ifedha ambazo zinatuamini na kutuwezesha kulima zao hili” Amesema Kayoza.

Akihitimisha kikao hicho mwenyekiti wa Chama cha Msingi Uyogo Maganga Jerome amesisitiza wakulima kufunga tumbaku kwa kufuata madaraja na kuepuka kuchanganya na uchafu ili kuifanya tumbaku kutoka Kahama iwe katika ushindani wa soko la kimataifa.

“Mwisho kabisa wakulima wangu tuzingatie kufunga tumbaku zetu kwa kufuata madaraja,na wenye tabia ya kuweka na uchafu waache tunataka tumbaku yetu toka Kahama iwe a Ushindani katika soko la kimataifa” Amesema Jerome.

Katika kikao hicho chama cha msingi Uyogo kimepitisha makubaliano ya Soko la tumbaku katika msimu wa huu kilimo yafanyike katika eneo lao laz uzalishaji ili kukwepa usumbufu wa kusafirisha zao hilo nje ya eneo lao la kilimo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *