POLISI YAWASHIKILIA WAWILI KWA TUHUMA ZA MAPENZI YA JINSIA MOJA.

Jeshi la Polisi Tanzania, Mkoa wa Mtwara linawashikilia watuhumiwa wawili ambao ni Dickson Paul Tamba (27) mjasiriamali mkazi wa mkuti chini machinjioni Wilaya ya Masasi na Mohamed Ally Kajao (34) Mwalimu Shule ya Msingi Nanyani, mkazi wa magomeni Wilaya ya Mtwara kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Tukio hilo limeripotiwa kufanyika mwezi Januari 2025 katika nyumba ya kulala wageni (jina limehifadhiwa) mara baada ya Dickosn Paul Tamba kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na Mohamed Ally Kajao, kunakili picha mjongeo kisha kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *