POLISI YAWAKAMATA WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA RELI NA TANESCO.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wenye asili ya Asia katika kijiji cha Kisemvule, Kata ya Vikindu, Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Kipolisi Rufiji, waliohujumu miundombinu ya TANESCO kwa kuiba nyaya za Copper zinazopatikana kwenye Transfomer za shirika hilo pamoja na kuharibu miundombinu ya Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa katika kiwanda chao ambapo walikuwa wamehifadhi mzigo wa nyaya za Copper zenye uzito wa Kilogramu 608.6 ambazo ni mali ya Tanesco pamoja na Copper Blocks 69 zenye uzito wa Kilogramu 5500.17 zilizotengenezwa baada ya kuyeyushwa kwa nyaya za Copper na kupata bidhaa nyingine ambayo inakiwango cha chini ili kuficha uhalisia, pamoja na Kilogramu 37 za nyaya za Copper mali ya shirika la Reli Tanzania.

Polisi Rufiji ilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine nane (8) wanaume ambao ni washirika wa watuhumiwa wa mwanzo katika kufanikisha hujuma za kuharibu miundombinu ya TANESCO na Shirika la Reli Tanzania kwa kuiba nyaya za Copper za mashirika hayo. Watuhumiwa hao walikutwa na nyaya za Copper Kilogramu 3, risiti mbalimbali za ununuzi wa nyaya za Copper, betri 7 za minara ya simu na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni ishirini na tano za kitanzania (25,000,000/-). Watuhumia wote 10 wameshafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *