Watu wanne wamepoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Kijiji cha Kiwanga wilaya ya Rufiji Mkoa wa Kipolisi Rufiji, katika barabara Kuu ya Kilwa – Dar es Salaam ikihusu Basi la abiria mali ya Kampuni ya Buti la Zungu aina ya Higer, lenye namba za usajili T 574 DZY lililokowa likiendeshwa na Mwalimu Selemani Shea (53), ambaye amevunjika miguu yote miwili.
Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, imeeleza kuwa basi likiwa na abiria 53 lilikuwa likitokea Kilwa Masoko Mkoa wa Lindi kuelekea jijini Dar es salaam, ambapo liliacha njia na kutumbukia kwenye daraja/kalavati na kupinduka na kusababisha vifo vya abiria hao wanne wote wanaume.



