Mtu mmoja, Rauli Mahabi mkazi wa Kurasini jijini Dar es Salaam, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kuhusiana na tukio la kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Padre Charles Kitima.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, imeeleza kuwa tukio hilo limetokea Aprili 30, 2025 majira ya saa nne usiku maeneo ya Baraza la Maaskofu Tanzania Kurasini Temeke Dar es salaam.

“Padri huyo tangu saa tatu asubuhi walikuwa na kikao na viongozi wa dini mbalimbali na baada ya kikao kuisha saa 1 jioni alikwenda kwenye kantini hadi saa nne na robo alipokwenda maliwatoni ndipo alidai kushambuliwa kichwani na kitu butu na watu wawili,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa Padri Kitima alipelekwa Hospitali ya Agakhan na anaendelea vizuri na matibabu na kwamba chunguzi wa kina unaendelea, ili hatua kali na za haraka zichulikuliwe kwa wahusika.
