Ofisi za chama cha FDC katika Wilaya ya Rukungiri zimefungwa na kuzingirwa na vikosi vya usalama, wakiwemo maafisa wa UPDF na Maafisa wa Polisi wa Uganda.
Wanachama hao, walikuwa wamepanga kufanya mkutano na Waandishi wa Habari ili kujadili hatma ya kuendelea kuzuiliwa kwa Dkt. Kizza Besigye ambaye ndiye muasisi wa FDC.

Besigye anaendelea kuzuiliwa pamoja na Hajj Obeid Lutale, kufuatia Serikali kuchelewa kutekeleza uamuzi wa Mahakama ya Juu wa Januari 31, 2025 uliosimamisha kesi za kiraia katika mahakama za kijeshi.
Wawili hao walikamatwa jijini Nairobi, Kenya Novemba mwaka 2024 na kushtakiwa kwa uhaini, kumiliki silaha na risasi kinyume cha sheria.
