Polisi wamuonya Bobi Wine

Polisi nchini Uganda wamepiga marufuku mikutano ya kisiasa inayoandaliwa na kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, kutokana na ukiukaji wa utaratibu wa umma na kumchafua Rais.

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi nchini humo, Bwn Tumusiime Katsigazi alisema mtu mmoja amefariki na wengine 10 kujeruhiwa vibaya katika mikutano ya chama cha National Unity Platform (NUP), wiki hii. Na amewaonya wafuasi wa NUP dhidi ya kile alichokitaja kuwa “mawazo ya kundi la watu…dhidi ya raia na wasimamizi wa usalama” na kusema Bobi anachochea makundi katika mikutano yake iliyoanza Jumatatu ya Septemba 11.

Hata hivyo Bobi Wine ameapa kuendelea na mikutano na kuwataka wafuasi wake kusubiri kauli yake ya kufanya mikutano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *