Polisi wakana kumkamata Naira Marley

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Jeshi la Polisi la Nigeria-Lagos, imekanusha taarifa iliyosambaa mitandaoni inayodai kuwa promota wa muziki, Sam Larry na Naira Marley, wamekamatwa kufuatia kifo cha mwimbaji Mohbad aliyefariki wiki hii.

Kupitia Msemaji wake wa mjini Lagos, Oluniyi Ogundeyi, amefunguka kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote ni uongo mtupu , msemaji amesema hayo kupitia mahojiano aliyofanya na mtandao wa Punch.

“Ripoti hiyo ni ya uongo; ni uongo; hakuna aliyekamatwa. Polisi hawakumkamata Naira Marley au Sam Larry.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *